Tundu Lissu asalia mikononi mwa polisi Tanzania

Maelezo ya sauti, Tundu Lissu asalia mikononi mwa polisi Tanzania
Tundu Lissu asalia mikononi mwa polisi Tanzania

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania (Chadema) kimesema kuwa kiongozi wake mkuu, Tundu Lissu anaendelea kushikiliwa na polisi baada ya kukamatwa Jumatano jioni alipomaliza kuhudhuria mkutano wa hadhara kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Chadema, Brenda Rupia kupitia mtandao wa X ameeleza kuwa wmepata taarifa za uhakika kuwa Lissu anasafirishwa na polisi kutoka mkoani Ruvuma na kupelekwa Dar Es Salaam.

Hata hivyo, mpaka kufikia sasa polisi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo na BBC inaendelea na juhudi za kuwatafuta.

Awali katika matangazo ya Amka na BBC yaliyoruka asubuhi hii, mwandishi mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili Florian Kaijage alieleza kwa undani tumachokifahamu kuhusu tukio hilo. Sikiliza.