'Walidhani nitajifungua mtoto mwenye ulemavu sawa na wangu'

Maelezo ya video, 'Walidhani nitajifungua mtoto mwenye ulemavu sawa na wangu'
'Walidhani nitajifungua mtoto mwenye ulemavu sawa na wangu'
  • Author, Fardowsa Hanshi
  • Nafasi, BBC News

Kwa miongo kadhaa watu wanaoishi na ulemavu nchini Somalia wamekabiliwa na ubaguzi, kutengwa, na ufikiaji mdogo wa haki za kimsingi za binadamu.

Asilimia kumi na moja (11%) ya watu wazima nchini humo wanaishi na ulemavu-ambao baadhi yao walijeruhiwa wakati wa mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabab wakati wa miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wamehangaika kutafuta kazi, kupata elimu, na kushiriki katika siasa.

Hata hivyo, sheria mpya ya kitaifa ya kuwalinda waalemavu, inaahidi kubadilisha hilo kwa kuhakikisha kuwa wanatambuliwa kisheria na kujumuishwa zaidi katika masuala ya kitaifa.

Lakini wanaharakati wanasema changamoto halisi sasa ipo katika utekelezaji.

Mwandishi wa BBC Fardowsa Hanshi, amerejea kutoka Mogadishu na kutuandalia taarifa ifuatayo.