Mashambulizi ya Israel huko Gaza 'yanavuka mipaka ya kinachohitajika' kukabiliana na Hamas - EU
Israel inasema kuwa lengo lake ni kuangamiza Hamas na kuwarejesha mateka wanaoshikiliwa na kundi hilo.
Muhtasari
- Salah: Ninaweza kucheza hadi niwe na umri wa miaka 40
- Daktari wa upasuaji aliyewalawiti mamia ya watu ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
- Makumi wajeruhiwa huku Wapalestina wakigombania msaada wa chakula Gaza - UN
- Arsenal ya Arteta haijafaulu vizuri - Henry
- Mfadhili wa mbegu kiume aliyezalisha watoto wenye saratani achochea miito ya mageuzi kuhusu ufahili wa mbegu za uzadi
- Namibia yaadhimisha mauaji ya kimbari ya kikoloni kwa mara ya kwanza
- Aliyemuua bwanaharusi kwa bomu ahukumiwa kifungo cha maisha jela nchini India
- Politico: Trump bado hajaamua hatua itakayochukua dhidi ya Urusi
- Marekani inasitisha miadi ya visa za wanafunzi
- Diddy alimteka nyara msaidizi wa zamani katika njama ya kumuua Kid Cudi - shahidi
- Ukraine inajenga shule 200 za chini ya ardhi - Mamlaka
- Trump: 'Putin anacheza na moto'
- Umati wa watu wavamia eneo jipya la usambazaji misaada huko Gaza
Moja kwa moja
Na Asha Juma & Dinah Gahamanyi
Mashambulizi ya Israel huko Gaza 'yanavuka mipaka ya kile kinachohitajika' kukabiliana na Hamas- EU
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, amesema kuwa "mashambulizi ya Israel huko Gaza yanavuka mipaka ya kile kinachohitajika kukabiliana na Hamas" huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka.
Kallas pia anasema kuwa EU haikuunga mkono mtindo mpya wa usambazaji wa misaada unaoungwa mkono na Marekani na Israel ambao haujumuishi Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu.
"Hatuungi mkono ubinafsishaji wa usambazaji wa misaada ya kiutu. Misaada ya kibinadamu haiwezi kutumiwa kama silaha", alisema.
Mashambulizi ya anga ya Israel na hatua zingine za kijeshi tangu kuanza tena kwa vita mnamo Machi kufuatia kusitishwa kwa mapigano yamesababisha vifo vya watu 3,924, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema.
Israel inasema kuwa lengo lake ni kuangamiza Hamas na kuwarejesha mateka wanaoshikiliwa na kundi hilo.
Kauli ya Kallas yanakuja baada ya Kansela mpya wa Ujerumani Friedrich Merz kusema kuwa "haelewi tena" malengo ya Israel katika eneo hilo lililozingirwa.
"Mbinu ambayo inawahangaisha raia... haiwezi tena kuhalalishwa kuwa mapambano dhidi ya ugaidi wa Hamas," alisema.
EU ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa misaada ya kibinadamu kwa Gaza, lakini Kallas alisema sehemu kubwa ya misaada hiyo haiwezi kuwafikia Wapalestina wanaohitaji.
Israel ilizuia misaada kuingia Gaza mnamo mwezi Machi na ilianza hivu majuzi kuruhusu kufika eneo hilo..
Unaweza pia kusoma:
Salah: Ninaweza kucheza hadi niwe na umri wa miaka 40
Chanzo cha picha, Reuters
Mchezaji wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah amesema anaweza kucheza hadi atakapofikisha umri wa miaka 40 na bado yuko kwenye mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuhamia Ligi ya Wataalamu ya Saudia.
Mshambulizi huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 32 alikuwa na msimu mzuri sana, akifunga mabao 29 na kutoa usaidizi katika kufungwa kwa mabao 18 huku Wekundu hao wakitwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Vyanzo vya habari viliiambia BBC kwamba Salah alikuwa akikaribia kupokea angalau pauni milioni 500 nchini Saudi Arabia kabla ya kuamua kuongeza mkataba wake na Liverpool mwezi uliopita.
Akizungumza na kituo cha ON Sport cha Misri, kabla ya mashabiki kadhaa wa Liverpool kujeruhiwa baada ya gari kugongana na umati wa watu waliokuwa wakisherehekea taji la ligi ya klabu hiyo Jumatatu, Salah alisema, "Nitaacha kucheza nitakapojisikia."
"Ukiniuliza, nadhani naweza kucheza hadi niwe na umri wa miaka 39 au 40, lakini nikijisikia kuacha kabla ya hapo, nitaacha. Nimepata mafanikio mengi," Salah alisema.
"Mkataba wangu na Liverpool ulikuwa unakaribia kuisha, na nilikuwa naenda Saudi Arabia, lakini tulikamilisha mkataba na Liverpool," alieleza.
Salah amefunga mabao 186 ya Primia Ligi katika timu za Liverpool na Chelsea, na yuko nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote, bao moja pekee nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa Newcastle na Manchester United Andrew Cole.
Unaweza pia kusoma:
Daktari wa upasuaji aliyewalawiti mamia ya watu ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Aliyekuwa daktari wa upasuaji wa Ufaransa Joel Le Scouarnec amekiri kuwadhulumu mamia ya wagonjwa kingono Aliyekuwa daktari wa upasuaji wa Ufaransa Joel Le Scouarnec amekiri kuwadhulumu mamia ya wagonjwa kingono
Joel Le Scouarnec, daktari wa upasuaji wa zamani ambaye amekiri kuwanyanyasa kingono mamia ya wagonjwa, wengi wao wakiwa watoto, kati ya mwaka 1989 na 2014 amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Le Scouarnec alikuwa amevalia nguo nyeusi alipokuwa amesimama bila hisia mahakamani akimsikiliza jaji Aude Burési akitoa uamuzi huo. Alikuwa amekiri mashtaka mwezi dhidi yake mwezi Machi.
Jaji Burési alisema mahakama ilizingatia ukweli kwamba daktari wa upasuaji wa zamani alikuwa akiwalenga zaidi waathiriwa wasio na afya, walio hatarini na waliotulia.
Le Scouarnec, mwenye umri wa 74, ametajwa kuwa mzazi mwenye watoto wengi zaidi nchini Ufaransa. Tayari yuko jela baada ya kuhukumiwa mwezi Disemba mwaka 2020 hadi miaka 15 kwa kubaka na kuwadhalilisha kingono watoto wanne, wakiwemo wapwa zake wawili.
Daktari huyo wa zamani amekuwa akishtakiwa huko Brittany tangu mwishoni mwa Februari.
Wakati huo makumi ya waathiriwa wake wametoa ushahidi, wakiiambia mahakama jinsi unyanyasaji waliopata wakiwa watoto ulivyobadilisha maisha yao.
Mnamo Machi, wakati wa kikao cha mahakama cha faragha, Le Scouarnec alikiri kuwadhulumu kingono waathiriwa wote 299, wengi wakati wamepigwa sindano ya ganzi [nusu kaputi), wanapoamka baada ya upasuaji.
"Siwezi tena kujiangalia kwa njia sawa kwa sababu mimi ni mlawiti na mbakaji wa watoto," Le Scouarnec alisema wakati wa taarifa zake za mwisho kwa mahakama wiki iliyopita.
"Mambo mengi yamesemwa. Si lazima nikumbuke kila kitu sasa. Bila shaka yatanirudia nikiwa kwenye maha yangu, lakini nilichoshuhudia [mahakamani] ni mateso ambayo ninahusika nayo," alisema.
Unaweza pia kusoma:
Makumi wajeruhiwa huku Wapalestina wakigombania msaada wa chakula Gaza - UN
Chanzo cha picha, Reuters
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inaamini kuwa watu 47 walijeruhiwa huko Gaza wakati umati wa watu ulipofurika kituo cha kusambaza misaada kinachoendeshwa na kundi jipya lenye utata linaloungwa mkono na Marekani na Israel.
Afisa mkuu alisema Umoja wa Mataifa bado unakusanya taarifa lakini wengi wa walijeruhiwa kutoka na milio ya risasi na kwamba "ilikuwa ni risasi kutoka kwa IDF [Israel Defence Forces] au la".
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema mtu mmoja aliuawa na wengine 48 kujeruhiwa.
Maelfu ya Wapalestina wamevamia kituo kusini mwa Gaza ambapo wakfu unaoungwa mkono na Marekani na Israel unasambaza misaada.
Baadhi ya video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha eneo hilo likiwa na vumbi huku uporaji huo ukifanyika.
Askari waliokuwa eneo la tukio walifyatua risasi hewani ili kuwatawanya watu hao na kuleta utulivu wa hali ya juu ili misaada isambazwe kwa utaratibu mzuri.
Wakfu mpya unaosambaza misaada umeupita Umoja wa Mataifa, ambao umekataa hatua zake, ukisema unakiuka sheria.
Mashirika kadhaa ya misaada yanasema kuna njaa kali huko Gaza baada ya Israel kuzuia misaada yote kuingia ndani ya Gaza kwa muda wa miezi 11, ikiwa ni sehemu ya mapambano yake dhidi ya Hamas.
Unaweza pia kusoma:
Arsenal ya Arteta haijafaulu vizuri - Henry
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Thierry Henry ndiye mfungaji bora wa Arsenal akiwa na mabao 228 Arsenal haijapata mafanikio chini ya meneja Mikel Arteta katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, anasema nahodha wa zamani Thierry Henry.
Arteta, 43, amewabadilisha The Gunners tangu kuondoka Manchester City na kujiunga na klabu hiyo mwaka 2019, na kuifanya timu hiyo kuwa na changamoto ya mataji mara kwa mara.
Lakini klabu hiyo haijashinda taji tangu ilipoifunga Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA wakati wa msimu wa kwanza wa Arteta kuinoa 2020.
Arsenal wamemaliza katika nafasi ya pili katika misimu mitatu iliyopita ya Primia Ligi, na walitolewa katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Carabao msimu huu.
"Sisemi kwamba nimekatishwa tamaa na Arsenal, lakini ni kawaida kwamba watu wanazua maswali sasa juu ya kile timu inachokifanya," Henry alikiambia kipindi cha Podcast ya Stick to Football.
Unaweza pia kusoma:
Mfadhili wa mbegu kiume aliyezalisha watoto wenye saratani achochea mageuzi ya ufadhili wa uzazi
Chanzo cha picha, Science Photo Library
Mbegu za uzazi za mwanamume mwenye mabadiliko ya nadra ya jeni inayohusishwa na saratani ziilitumiwa kupata watoto wengi kote Ulaya, na hivyo kusababisha wito wa udhibiti zaidi na kikomo cha idadi ya waroro inayoruhusiwa kutoka kwa mfadhili mmoja.
Mbegu za kiume za uzazi kutoka kwa mfadhili mmoja zilitumiwa kupata angalau watoto 67 kutoka kwa familia 46 waliozaliwa kati ya 2008 na 2015, alisema Edwige Kasper, mwanabiolojia katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Rouen nchini Ufaransa, wakati wa mada katika mkutano wa kila mwaka wa Jumuiya ya Ulaya ya Jeni ya urithi ya Binadamu huko Milan Jumamosi. Kumi kati ya watoto hao tayari wamepatikana na saratani.
"Katika kiini cha tatizo inaonekana kuwa hakuna udhibiti, au pengine ukosefu wa udhibiti, wa idadi ya watoto wanaozaliwa na mfadhili mmoja," alisema.
Uchambuzi ulionyesha kuwa mfadhili huyo ambaye mwenyewe ni mzima wa afya alikuwa na mabadiliko ya nadra katika jeni inayoitwa TP53, ambayo huenda ikasababisha ugonjwa wa Li-Fraumeni, ugonjwa adimu unaoongeza hatari ya mtu kupata saratani.
Mabadiliko hayakujulikana wakati mchango huo ulitolewa, lakini watoto waliozaliwa kutoka kwa mfadhili huyo wametambuliwa katika nchi nane tofauti za Ulaya: Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Uhispania, Uswidi na Uingereza, alisema Kasper katika mada yake.
Unaweza pia kusoma:
Namibia yaadhimisha mauaji ya kimbari ya kikoloni kwa mara ya kwanza
Chanzo cha picha, Ullstein Bild / Getty Images
Maelezo ya picha, Mauaji ya halaiki katika eneo ambalo sasa ni Namibia yalidumu kuanzia 1904 hadi 1908 Yanayoitwa "mauaji ya kimbari yaliyosahaulika ya Ujerumani", na yanaelezwa na wanahistoria kama mauaji ya halaiki ya kwanza ya Karne ya 20, mauaji ya kimfumo ya zaidi ya Waafrika 70,000 yanaadhimishwa kwa siku ya kumbukumbu ya kitaifa kwa mara ya kwanza nchini Namibia.
Karibu miaka 40 kabla ya kutumika katika Maangamizi Makubwa ya Wayahudi, kambi za mateso na majaribio ya kisayansi ya uwongo yalitumiwa na maofisa wa Ujerumani kutesa na kuua watu katika ile iliyokuwa ikiitwa wakati huo Afrika Kusini Magharibi.
Waathiriwa ambao hasa n kutoka kwa jamii za Ovaherero na Nama, walilengwa kwa sababu walikataa kuwaruhusu wakoloni kuchukua ardhi na ng'ombe wao.
Siku ya Kukumbuka Mauaji ya Kimbari nchini Namibia Jumatano inafuatia miaka ya shinikizo kwa Ujerumani kuitaka ilipe fidia.
Siku hiyo mpya ya mapumziko ya kitaifa itaadhimishwa kila mwaka kama sehemu ya "safari ya uponyaji" ya Namibia ikiwa ikiambatana na kukaa kimwa kwa kwa dakika moja na mkesha wa kuwasha mishumaa nje ya bunge mjini Windhoek, kulingana na serikali.
Kwa miaka mingi Ujerumani haikukiri hadharani mauaji makubwa yaliyotokea kati ya 1904 na 1908.
Lakini miaka minne iliyopita ilitambua rasmi kwamba wakoloni wa Kijerumani walifanya mauaji ya halaiki, na kutoa €1.1bn (£940m; $1.34bn) kama msaada wa maendeleo utakaolipwa kwa zaidi ya miaka 30 - bila kutaja "fidia" au "fidia" katika maneno ya kisheria.
Unaweza pia kusoma:
Aliyemuua bwanaharusi kwa bomu ahukumiwa kifungo cha maisha jela nchini India
Maelezo ya picha, Sahu aliuawa na mkewe Reema kujeruhiwa vibaya na bomu lililofichwa kwenye zawadi ya harusi Aliyekuwa mkuu wa chuo katika jimbo la mashariki mwa India la Odisha amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kutuma bomu lililomuua mwanamume aliyeoana hivi karibuni na shangazi yake mnamo 2018.
Mahakama ilimpata Punjilal Meher, 56, na hatia ya kuua, kujaribu kuua, na kutumia vilipuzi katika kesi iliyojulikana kama "bomu la harusi" , kesji iliyoishangaza India.
Bomu hilo, lililofichwa kama zawadi ya harusi, lilifikishwa nyumbani kwa Soumya Sekhar Sahu, mhandisi wa programu za kompyuta mwenye umri wa miaka 26, siku chache baada ya harusi yake.
Wenzi hao walipofungua kifurushi hicho, kililipuka - na kumuua Sahu na shangazi yake mkubwa, na kumwacha mkewe, Reema, ambaye alifungua kifurushi hicho, akiwa amejeruhiwa vibaya.
Chanzo cha picha, Facebook/Punji Lal Mehe
Maelezo ya picha, Punjilal Meher alipatikana na hatia ya mauaji, jaribio la kuua, na matumizi ya vilipuzi Huku ikikubali hoja ya mwendesha mashitaka kwamba ilikuwa ni jinai "mbaya", mahakama ilikataa kuainisha kama kesi " ya nadra kati ya " inayostahili hukumu ya kifo.
BBC iliangazia tukio hilo katika mfululizo wa kina wa sehemu mbili za uchunguzi.
Wachunguzi walisema kuwa Meher alikuwa na kinyongo kuhusu ushindani wa kitaaluma na alipanga shambulio hilo kwa umakini.
Alitumia jina na anwani ya uongo kutuma bomu kutoka Raipur, akichagua huduma ya kutuma barua bila CCTV au kuchanganua vifurushi.
Unaweza pia kusoma:
Politico: Trump bado hajaamua hatua atakayochukua dhidi ya Urusi
Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba uvumilivu wake kwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin umepungua, lakini bado hajaamua nini cha kufanya, Gazeti la Politico limeripoti.
"Putin anakaribia kuharibu fursa adimu ambayo Trump amempatia," afisa mmoja wa utawala wa Marekani aliambia gazeti hilo kwa sharti la kutotajwa jina.
Trump bado hajaamua iwapo ataiwekea Moscow vikwazo zaidi ili kukabiliana na mashambulizi makali ya Urusi dhidi ya Ukraine, kwa mujibu wa maafisa wanne wa Marekani.
"Nina mashaka sana hivi sasa kwamba Trump ataiwekea Urusi vikwazo au kuichukulia hatua kali," alismea Kurt Volker, ambaye aliwahi kuwa mjumbe maalum wa Marekani nchini Ukraine wakati wa muhula wa kwanza wa Trump. "Amekuwa na fursa nyingi sana za kufanya hivi, lakini kila mara ameziepuka."
Soma zaidi:
Marekani inasitisha miadi ya viza za wanafunzi
Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeziamuru balozi za Marekani kuacha kupanga ratiba ya viza za wanafunzi huku ikijiandaa kupanua uhakiki wa waombaji kama hao kwenye mitandao ya kijamii.
Katika nakala iliyotumwa kwa nyadhifa za kidiplomasia, Katibu wa Jimbo Marco Rubio alisema mchakato huo utasitishwa "hadi mwongozo zaidi utakapotolewa".
Ujumbe huo ulisema ukaguzi wa mitandao ya kijamii utaimarishwa kwa visa za wanafunzi, jambo ambalo litakuwa na "madhara makubwa" kwa balozi na balozi ndogo.
Hatua hii inachukuliwa huku kukiwa na mzozo wa Trump na baadhi ya vyuo vya wasomi zaidi Marekani, ambavyo anaamini vina mrengo wa kushoto sana. Anasema baadhi yao wamewezesha chuki dhidi ya Wayahudi chuoni na kushikilia sera za ubaguzi.
Nakala ya idara ya serikali, iliyotazamwa na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News, ilielekeza balozi za Marekani siku ya Jumanne kuondoa miadi yoyote ambayo haijajazwa kwenye kalenda zao kwa wanafunzi wanaotafuta visa, lakini ilisema wale walio na miadi tayari na imepangwa wanaweza kuendelea.
Pia ilisema idara ya serikali ilikuwa ikijiandaa kwa "upanuzi wa uchunguzi na ukaguzi wa mitandao ya kijamii" unaotumika kwa maombi yote ya visa ya wanafunzi.
Soma zaidi:
Diddy alimteka nyara msaidizi wa zamani katika njama ya kumuua Kid Cudi - shahidi
Chanzo cha picha, Getty Images
Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa Sean 'Diddy' Combs' ametoa ushahidi kwamba msanii huyo wa muziki wa hip-hop alimteka nyara kwa mtutu wa bunduki, kisha kuingia nyumbani kwa rapa Kid Cudi kwa njama ya kumuua.
Capricorn Clark, ambaye alifanya kazi na Bwana Combs kwa zaidi ya muongo mmoja, aliiambia mahakama kwamba mshtakiwa na mlinzi walifika kwenye nyumba yake mwaka 2011 na kumlazimisha kuendesha gari pamoja nao hadi nyumbani kwa Kid Cudi.
"Vaa nguo," alikumbuka Bw Combs akisema. "Tunaenda kumuua huyu [alitumia neno la matusi]." Pia aliiambia mahakama kwamba Diddy alitishia kumuua katika siku yake ya kwanza kabisa kufanya kazi nyumbani kwake.
Bw Combs, 55, amekana mashtaka ya ulaghai, ulanguzi wa ngono na usafirishaji ili kujihusisha na ukahaba.
Soma zaidi:
Ukraine inajenga shule 200 za chini ya ardhi - Mamlaka
Chanzo cha picha, Reuters
Ukraine inapanga kujenga shule zipatazo 180 za chini ya ardhi kufikia mwisho wa mwaka 2025, alisema Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal, kwenye kongamano la "Elimu ya Ukraine Mpya" huko Kyiv.
Maneno yake yamenukuliwa na Interfax-Ukraine ikisema kuwa vituo 15 vya mafunzo ya chini ya ardhi tayari vimejengwa.
Kulingana na Shmyhal, kwa sasa 80% ya shule zote za Ukraine zina makazi ya aina mbalimbali.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi wa Ukraine Oleksiy Kuleba, zaidi ya majengo 4,000 ya shule, shule za ufundi na taasisi nyingine za elimu zimeorodheshwa katika sajili ya yale yaliyoharibiwa.
Soma zaidi:
Trump: 'Putin anacheza na moto'
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani Donald Trump alisema ameiokoa Urusi kutokana na "mambo mengi mabaya sana."
"Vladimir Putin hatambui kwamba ikiwa sio mimi, mambo mengi mabaya yangekuwa yametokea Urusi kufikia sasa," aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social, bila kutoa maelezo ya kina.
"Anacheza na moto!" - Trump aliongeza.
Siku moja kabla, baada ya siku tatu za mashambulizi makubwa ya makombora ya Urusi na ndege zisizo na rubani katika miji ya Ukraine na kuua raia 12, rais wa Marekani alimkosoa vikali Putin, ambaye Trump alisema "amekuwa mwendawazimu" kwa kuua watu "kiholela".
Jarida la Wall Street Journal limegundua kuwa Trump anafikiria kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi.
Ikulu ya Urusi ilisema Trump "anaendeshwa na hisia."
Soma zaidi:
Umati wa watu wavamia eneo jipya la usambazaji misaada huko Gaza
Chanzo cha picha, Reuters
Maelfu ya Wapalestina wamevamia eneo la kusambaza misaada huko Gaza lililoanzishwa na kundi lenye utata linaloungwa mkono na Marekani na Israel, siku moja baada ya kuanza kufanya kazi katika eneo hilo.
Video zilionyesha umati wa watu wakitembea juu ya uzio uliobomolewa kwenye kambi ya Wakfu wa Gaza Humanitarian Foundation (GHF) katika mji wa kusini wa Rafah.
Kundi hilo lilisema kuwa wakati fulani timu yake ilirudi nyuma kwa sababu idadi ya wanaotaka msaada ilikuwa kubwa sana. Jeshi la Israel lilisema wanajeshi waliokuwa karibu walifyatua risasi za onyo.
GHF, ambalo linatumia wanakandarasi wa usalama wa Marekani wenye silaha, inalenga kuukwepa Umoja wa Mataifa kama msambazaji mkuu wa misaada huko Gaza, ambapo wataalam wameonya kuhusu njaa kubwa baada ya zuio la wiki 11 la Israel kuondolewa hivi karibuni.
Umoja wa Mataifa ulisema video hizo kutoka kwa Rafah "zinavunja moyo" na kwamba ina mpango wa kina wa kupata msaada wa kutosha kwa "watu waliokata tamaa" milioni 2.1.
Umoja wa Mataifa na mashirika mengi ya misaada yamekataa kushirikiana na mipango ya GHF, ambayo wanasema inakinzana na kanuni za kibinadamu na inaonekana kutumia "msaada kama silaha".
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja.